Kifaru cha jeshi (JWTZ) pata ajali huko Lindi

. . Hakuna maoni:

Kutoka Lindi kuna taarifa ambayo imethibitishwa
pia na kamanda Mpinga kuhusu ajali iliyotokea
Mtwara ambayo imehusisha gari la Jeshi la
Wananchi Tanzania(Jwtz)imeripotiwa asubuhi ya
leo na shuhuda wa eneo hilo.


Msafara huo wa Wanajeshi ulikuwa ukitokea
Mtwara kuelekea Nachingwea kwenye camp
kubwa ya Jeshi na ajali hiyo imetokea maeneo
ya Mnolela kijijini Lindi,kwa mujibu wa shuhuda
ambaye ametoa taarifa hii kupitia kipindi cha
Power Breakfast kutoka Clouds Fm amesema
ajali hiyo imeua wanajeshi 3 na mwenye
nyumba mmoja ambaye ni mwanamke alikua
kalala ndani.
Madhara mengine yaliyotokana na ajali hii ni
nyumba mbili kuharibika vibaya,majeruhi wa
ajali hii wamepelekwa kwenye hospital ya Mkoa
wa Mtwara.
Bonyeza play kumsikiliza shuhuda wa ajali hii.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Machapisho Maarufu